Hiki ni kituko; Huyu jamaa alipelekwa Mahakamani kwa kesi ya kubaka, alipofika Mahakamani akataka kumbaka mtu tena
Hii ni stori nyingine tena ya 2014 ambayo inaingia kwenye list ya
zile stori ambazo ukishaisoma au kuipata unaanza kufikiria mara
mbilimbili na kujaribu pia kutengeneza picha yako mwenyewe kama upo eneo
la tukio.
Watu wa karibu wa Mtuhumiwa huyu walijitokeza Mahakamani ili kuangalia kama ndugu yao aitwae Simon Ngozi (21) ataweza kupata dhamana kwenye kesi inayomkabili ya kubaka mtoto wa miaka tisa.
Imetokea Kenya ambapo jamaa alikua amepelekwa Mahakamani Makadara Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.

Shughuli za Mahakama zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka sakafuni
Baada ya hapo dada wa mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya ubakaji.
Post a Comment: