48 wauawa katika mashambulizi Lamu-Kenya

Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Kiislamu wameshambulia
kituo cha polisi na mahoteli na vijiji mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi
wakitorokea maeneo ya msitu karibu na kisiwa cha Lamu..
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48
wanahofiwa kuuawa kartika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi lilifanyika usiku wa kuamkia leo watu waliokuwa wamejifunika nyuso
zao wakiwa wamejihami vikali walivamia vituop vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga
ofisi zake kwa hofu ya usalama.
Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa
kundi gani.
Baadhi ya walioshuhudia wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi
wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al
Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika
malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha
wakavamia na kuiba silaha.
Kituo kimoja cha polisi kilichoshambuliwa na wapiganaji
hao
'Washambuliaji ni kina nani ?'
Msemaji wa Jeshi la Kenya Meja Emmanuel Chirchir ameandika katika mtandao wa
Twitter kusema kuwa wapiganaji hao wameshambulia kijiji kimoja na kufyatua
risasi kiholela katika kituo kikuu cha biashara.
''Huenda wapiaganji hao wakawa Al shabaab,'' ameongeza Major Chirhir.
Usiku wote ndege za polisi zimepaa eneo la Mpeketoni hadi Lamu kudadisi hali
ilivyo huku polisi wakikabiliana vikali ardhini. Kamanda mkuu wa kaunti ya Lamu
ameondoka na maafisa zaidi wa polisi kusaidia makabiliano yanayoendelea
huko.
Mmoja wa walioshuhudia amesema kuwa mahoteli yameshambuliwa. "baadhi ya
mahoteli yamewashwa moto hatujui watu wangapi wamejeruhiwa kufikia sasa.
Tumeambiwa wameshatoroka lakini polisi wanawafuata waliko,'' ameongeza.
Lamu , Kenya
'Kivutio cha watalii'
Kisiwa cha Lamu kilichoko karibu sana na eneo hilo ni maarufu sana kwa
shughuli za kitalii katika eneo hilo la Afrika, huku likiwa na majengo ya kale
zaidi na kihistoria ambayo yameorodheshwa na shirika la Unesco kama turathi ya
kimataifa.
Post a Comment: