Papa Francis amewapokea viongozi wa Israil na Palestina katika Vatikani.
2:07:00 PM
Rais Shimon Peres wa Israil na Mahmoud Abbas wa Palestina walikutana Vatikani kuomba amani Mashariki ya Kati.
Viongozi hao wawili walikutana na Papa nje ya
nyumba yake, kabla ya kusafiri pamoja naye na kiongozi wa kanisa la
Orthodox, Askofu Mkuu Bartholomew, hadi kwenye sherehe katika bustani ya
Vatikani.
Wakitarajiwa kupandisha mzaituni kama alama ya
kudumu ya hamu ya pande zote mbili ya kupata amani baina ya watu wa
Israil na Palestina.
Papa alisema yeye hataki kuhusika moja-kwa-moja
na mazungumzo ya amani, lakini anatumai viongozi hao wakikutana, huenda
ikasaidia kupunguza uhasama kati yao.
Post a Comment: