Rais Jacob Zuma alazwa hospitalini
1:41:00 PM
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa uchunguzi wa kiafya .
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa
ofisi yake. Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa
muda ingawa ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.
“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma
alishauriwa kupumzika hasa baada ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki
chache zilizopita.Madaktari hawajaeleza wasiwasi wowote kuhusu afya
yake.’’
Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati dhidi ya
utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa
pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC
kilishinda uchaguzi huo.
Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu
kukabiliana na uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha
pamoja na ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.
Post a Comment: