Mwanamume ajibandika urembo kufanana na Kim
Sura huonekana katika baadhi ya majarida maarufu duniani, ana kipindi
chake maalum kuhusu maisha yake na familia yake, ana kampuni ya vipodozi
na pia ana mamilioni ya dola kwenye akauti zake za benki. Si mwingine bali ni mwanadada Kim Kardashian ambaye yumo vinywani mwa watu wengi duniani.
Sio ajabu kama kuna mtu angetaka kufanana na yeye. Kutana na kijana Jordan James kutoka Uingereza mwenye umri wa miaka 23 ambaye ari yake maishani ni kufanana tu kama Kim Kardashian.
Mvulana huyu amefanya mambo ya ajabu akijitahidi kufanana na Kim kwa kujiongeza urembo bandia, hasa kufanya midomo yake kuwa mikubwa akitaka ifanane na ya Kim.
Je unajua ametumia kiwango gani cha pesa katika harakati zake za kutaka kufanana kama Kim? Pauni 150,000 au dola laki mbili na arobaini.Pesa hizo zote amezitumia kwa kufanyiwa upasuaji na kuongezwa urembo bandia.Cha kushangaza ni kwamba huyu ni mwanamume anayetaka kufanana kama mwanamke.
![]() |
| Jordan James hutumia mamia ya dola kujweka urembo bandia na kufanana kichekesho kwa wengi |

Post a Comment: