Watoto wazuiwa kuitembelea Israel
![]() |
| Watoto waliotekwa Gaza ndani ya Basi |
Kundi la Hamas limewazuia kundi la
watoto kutoka ukanda wa Gaza wengi wakiwa ni wale waliowapoteza wazazi
kwenye vita vya hivi majuzi kati ya Hamas na Israel waliotaka
kuitembelea Israeli katika ziara ambayo waandalizi wake wanasema
ililenga kuleta uwiano. Msemaji wa Hamas anasema kuwa ziara hiyo
ilizuiwa ili kulinda tamaduni ya watu wa ukanda wa Gaza.
Wapiganaji wa kundi la Hamas wamezuia kundi la watoto kutoka Gaza wengi wao wakiwa ni wale ambao wazazi wao waliuawa katika vita.
Wanaharakati wa
masuala ya Amani waliowasaidia watoto hao kufanya safari hiyo wamesema
kuwa mamlaka ya Gaza waliruhusu watoto hao kufanya safari yao lakini
wakabadili msimamo wao baadae.

Post a Comment: