DONALD TRUMP AWAKALIA KOONI REPUBLICANS
Wanachama wa chama cha Republicans nchini Marekani wametofautiana kuhusu kumuunga mkono mgombea wa urais wa chama hicho Donald Trump baada ya mfanyibiashara huyo kushinda uteuzi wa chama hicho.
Baadhi ya wanachama hao wameandika katika mitandao
ya kijamii kuhusu kujiondoa kwao katika chama hicho kupitia kuchoma
vibali vyao vya kupiga kura.
Hatahivyo wengine wameanza kumuunga
mkono mgombea huyo wakisema kuwa bw Trump anapendwa sana kushinda
Hillary Clinton ambaye anapigiwa upatu kushinda uteuzi wa chama cha
Demokrat.
Bwana Trump hana umaarufu mongoni mwa wapiga kura wengi nchini Marekani.
![]() | |
| Donald Trump akinadi sera zake kwa wamarekani |
''Iwapo tutamteua Trump,tutaharibikiwa na itakuwa
kupenda kwetu'',Seneta wa jimbo la Carolina Lindsay Grahama alisema siku
ya Jumanne baada ya Seneta wa Texas Ted Cruz kujiondoa katika
kinyang'anyiro hicho na hivyobasi kumpatia bw Trump fursa.
Wengine
kama vile aliyekuwa gavana wa jimbo la Louisiana Bobby Jindal ambaye
amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bw Trump katika siku za nyuma amesema kuwa
atamuunga mkono katika uchaguzi ujao.


Post a Comment: