HATIMAYE 'CHURA' WA SNURA KAZAMISHWA NA BASATA
Kwanzia tarehe May 04 2016 Wizara ya habari, utamaduni, sanaa na michezo wamekutana na waandishi wa habari na kutoa tamko la kuufungia wimbo wa Snura ‘chura’ kuchezwa kwenye MEDIA kuanzia leo mpaka hapo Snura atakapoifanyia marekebisho video ya wimbo huo na kutoa wimbo huo kwenye mitandao yote ya kijamii.
Source: http://millardayo.com
Sababu za
kuufungia ni kinachoonekana ndani ya video ambapo pia Serikali
imetangaza kusitisha maonyesho yote ya hadhara ya Snura mpaka
atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake za sanaa katika baraza
la sanaa la taifa BASATA.
Akizungumza Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, Zawadi Msalla aliieleza kuwa
'Serikali imesitisha wimbo na video ya chura kupigwa katika vyombo vyote vya habari, maeneo ya wazi na maeneo yote baada ya kuangalia na kuona miondoko iliyotumika katika utengenezaji wa video ile kwanza ni ya udhalilishaji, aina maadili ya mtanzania na ukiukwaji wa haki za binadamu’.

Post a Comment: