HATIMAYE Dkt MIGIRO ATEULIWA BAROZI WA TANZANIA UINGEREZA
Mmoja wa wanasiasa waliokuwa wakipigania tiketi ya kuwania urais kupitia chama cha CCM nchini Tanzania ameteuliwa kuwa balozi wan chi hiyo Uingereza.
Dkt Asha-Rose Migiro atachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw Peter Kallaghe ambaye amerejea nyumbani.
Anatarajiwa kuapishwa Alhamisi katika ikulu ndogo ya rais Dodoma.
Bi
Migiro alihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria serikali iliyopita na
alikuwa miongoni mwa wagombea watatu waliokuwa wamesalia kwenye
kinyang'anyiro cha kuteua mgombea wa CCM uchaguzi wa mwaka jana, kabla
ya mwishowe Dkt John Magufuli kuidhinishwa.
Mgombea huyo mwingine alikuwa Balozi Amina Salum Ali.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:
taarifa kwa vyombo vya habari
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu : +255-22-2114512, 2116898
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
Email : press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425

OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Dkt. Asha-Rose Migiro anakwenda kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kalaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Dkt. Asha-Rose Migiro ataapishwa kesho Alhamisi tarehe 05 Mei, 2016 katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
04 Mei, 2016
Source: Taarifa toka Ikulu


Post a Comment: