KAMA BADO HUKUIPATA HII: JUSTIN BIEBER ASHTAKIWA KWA KUVUNJA SIMU
Mwanamuziki Justin Bieber ameshtakiwa kwa dola milioni 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu.
Nyota
huyo ametuhumiwa kuivunja simu ya Robert Earl Morgan baada ya kujaribu
kumrekodi Bieber wakati alipokuwa akinywa pombeKIsa hicxho kilitokea
katika kilabu ya Cle mjini Texas mwezi uliopita.
Kulingana na mtandao wa TMZ,Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu yake na kuivunja.
Thamani ya iPhone haifiki dola 100,000.
Lakini
ameshtakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa
na picha ambazo haziwezi kupatikana tena,ikiwemo picha za sherehe ya
miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake.
Morgan pia anadai kwamba alipoteza idad kubwa ya nambari zake za mawasiliano ya biashara.
Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Kisa hicho
kinaaminika kufanyika jioni ambayo Bieber alionekana kumchoma na sigara
Post Malone,ambay amekuwa akimsaidia katika ziara yake ya duniani.
Picha
zilionekana siku chache baadaye zikimuonyesha Malone akiushika mkono wa
Bieber kabla ya kumshika shingo Nyota huyo wa muziki wa Pop.
Lakini mwanamuziki huyo baadaye alisema kuwa walikuwa wakifanya utani.


Post a Comment: