NEWS: Mpinzani wa Donald Trump, John Kasich ameamua kuachia ngazi
Mpinzani mkuu wa Donald Trump katika kinyang'anyiro cha tikiti ya urais wa chama cha Republican , John Kasich amejiondoa mashindanoni.
Gavana huyo wa jimbo la Ohio ametangaza kusitisha kampeini zake baada ya kura yamaoni kuonesha kuwa umaarufu wake hauwezi kumpiku bwenyenye huyo mbishi anayepigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania urais wa Marekani.
Bw Trump anapigiwa upatu kutawazwa mgombea wa Republican.
Kwa upande wake Kasich hakushinda jimbo lolote isipokuwa lake la Ohio.
Mpinzani mweza ambaye ni Seneta wa jimbo la Texas Ted Cruz naye alijiondoa mapema wiki hii kufuatia kushindwa kwake na bw trump katika jimbo la Indiana .
Gavana Kasich amefutilia mbali mikutano ya hadhara ya kampeini katika jimbo ya Washington. Mapema leo bw Kasich alizindua nembo yake iliyoundwa kwa mfano wa filamu maarufu ya Star-Wars ambapo alijieleza kuwa ndiye aliyesalia pekee yake dhidi ya Donald Trump.


Post a Comment: