TANZIA: Kijana Nihal Bilta aliyeugua ugonjwa wa kuzeeka aaga dunia.
![]() |
| Nihal Bilta |
Kijana mmoja wa mjini Mumbai ambaye amekuwa akiugua ugonjwa usio kawaida wa jeni ambao huufanya mwili kuzeeka mara nane zaidi ya ilivyo kawaida amefariki.
Nihal Bitla mwenye umri wa miaka 15 alikuwa mwanaharakati wa India anayefanya kampeni dhidi ya ugonjwa huo kwa jina Progeria.
Bitla
aligonga vichwa vya habari alipokuwa akitafuta wagonjwa wengine 60
wanaougua ugonjwa huo ili kushiriki katika yake mjini Boston.Alianzisha
mtandao wa kijamii kutoa hamasa kuhusu ugonjwa huo.
Hivi karibuni
alianzisha hamasa kwa jina #HatsOnProgeria,ambapo alionekana na kundi
moja la wafuasi wake katika kituo cha reli cha Chhatrapati Shivaji.
Bitla
alipata umaarufu baada ya kukutana na nyota wa Bollywood Aamir Khan
mnamo mwezi Disemba baada ya ukurasa wake wa facebook kuzungumzia kuhusu
habari yake na swala kwamba alikuwa shabiki mkubwa wa nyota huyo.
Alifariki hospitalini siku ya Jumanne kusini mwa jimbo la Telangana,ambapo alikuwa ameenda kuhudhuria sherehe za harusi.
Ripoti za vyombo habari zinasema kuwa huenda alikosa maji mwilini kutokana na joto katika eneo hilo.

Post a Comment: